Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI- HAWA GHASIA amewaagiza
Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala na Wakurugenzi wa mikoa ya LINDI na
MTWARA kuhakikisha inahamasisha wananchi kutumia chumvi iliyowekwa
madini joto ili kupunguza udumavu wa akili kwa watoto.
Akitoa agizo hilo mkoani LINDI wakati akifunga mafunzo ya Maafisa Lishe
kutoka Nchi nzima Waziri GHASIA amesema utumiaji wa chumvi isiyokuwa na
madini joto imeongezeka na kufikia asilimia 92 ambapo kushuka huko
kumechangiwa na mikoa ya LINDI na MTWARA.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wameipongeza serikali na kusema
wataenda kuhamasisha jamii umuhimu wa kutumia chumvi yenye madini joto.


Tags:
Habari za Kimataifa