RAIS JAKAYA KIKWETE ATOA ZAWADI YA PASAKA

Siku ya Ijumaa Kuu wakristo nchini waungana na wakristo wengine duniani kote kuadhimisha siku ya mateso ya Yesu Kristo msalabani. Katika kuadhimisha sikukuu ya PASAKA Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania JAKAYA KIKWETE ametoa zawadi ya pasaka kwa watoto katika mahabusu ya watoto ya MWANJELWA iliyopo katikati ya Jiji la MBEYA pamoja na gereza la watoto la IRAMBO lililopo tarafa ya TEMBELA wilaya ya MBEYA. Akikabidhi zawadi hizo kwa niaba ya Rais Mkuu wa wilaya ya MBEYA NYEREMBE MUNASASABI amesema ni ukarimu wa Rais KIKWETE kutambua jamii kama hizi ili zijione kuwa ni jamii kama jamii nyingine. Kwa upande wao walezi wa watoto hao wamemshukuru raisi KIKWETE kwa kuwakumbuka hasa kipindi hiki cha sikukuu

Post a Comment

Previous Post Next Post