Rais Kikwete
akijiandikisha kupiga kura Zaidi ya watanzania milioni kumi na moja
katika milioni ishirini na tano waliokusudiwa wamejitokeza kujiandikisha
kwenye daftari la kudumu la wapiga kura kwa kutumia mfumo wa mashine za
BVR licha ya changamoto kadha wa kadha zilizo jitokeza. Akisoma taarifa
ya zoezi hilo mbele ya raisi Jakaya Kikwete, aliyeungana na watanzania
wa mkoa wa Pwani kwenye kujiandikisha, mwenyekiti wa tume ya taifa ya
uchaguzi jaji mstaafu damiani lubuva,amesema taayari watanzania zaidi ya
milioni kumi na moja wamejiandikisha katika mikoa kumi na tatu huku
matarajiwa yakiwa ni watanzania milioni 24 wakitarajiwa, huku mikoa kumi
na moja ikiwa imesalia kukamilisha zoezi hilo. Raisi Jakaya Kikwete
amekuwa miongoni mwa watanzania waliojitikeza kujiandikisha katika
kijiji cha Msoga Bagamoyo mkoani Pwani, kwenye daftari la kudumu la
wapiga kura zoezi lililoanza kwenye mkoa huo, na kuipongeza tume kwa
kuendelea na zoezi hilo licha ya kugubikwa na changamoto kadha wa kadha
na kutoa wito kwa watanzania kuacha kulalamika mara baada ya uchaguzi
bila ya kujitokeza kujiandikisha na kupiga kura. Baadhi ya wananchi wa
Msoga waliojitokeza kujiandikish wameelezea changamoto ya huduma ya
umeme kwaaajili ya matumizi ya mashine za BVR, ambapo wamesema
watashirikiana kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa huku mbunge wa jimbo
la Chalinze mheshimiwa Ridhiwani Kikwete amewaomba wananchi kujitokeza
kujandikisha na kutumia haki yao ya msingi ya kikatiba. Copy and WIN :
http://ow.ly/KNICZ
Copy and WIN : http://ow.ly/KNICZ
Copy and WIN : http://ow.ly/KNICZ
Copy and WIN : http://ow.ly/KNICZ
Tags:
Habari za Kimataifa