Majeshi ya SAUDI ARABIA yaanza kuwashambulia HOUTH


Majeshi ya SAUDI ARABIA yaanza kuwashambulia HOUTHI Majeshi ya serikali ya SAUDI ARABIA, yameanza mashambulio dhidi ya wapiganaji wa kikundi cha HOUTHI cha nchini YEMEN, ikiwa ni hatua ya kuisaidia serikali ya rais wa YEMEN, ABDUL RABU MANSOUR HADI, inayoshambuliwa na kikundi hicho. SAUDI ARABIA imetangaza rasmi kuwa imeanza mashambulio dhidi ya wapiganaji hao, na tayari mapigano hayo yamesababisha vifo vya watu 17. Wapiganaji hao wanadai kuwa watu waliokufa katika mashambulio yaliyofanywa na SAUDI ARABIA ni raia. Wapiganaji wa kikundi cha HOUTHI kutoka katika madhehebu ya SHIA wamekuwa wakiendelea na mashambulio dhidi ya rasilimali za serikali nchini YEMEN. Wiki hii wapiganaji hao walitwaa uwanja wa ndege wa TAIZ, na kuteka moja kati ya kambi za kijeshi nchini humo. Wapiganaji hao wamekuwa wakiwashikilia viongozi mbalimbali wa serikali na kuwafunga kifungo cha nyumbani.

Post a Comment

Previous Post Next Post