chuo Kikuu
cha Dodoma, UDOM kimezindua
Mtambo wa kwanza wa aina yake barani
Afrika wa kuchunguza na kutafiti Miamba
yenye Madini, Mafuta na Gesi kwa ajili ya
kufundishia Wanafunzi wanaosoma Sayansi
Ardhi Chuoni hapo.
Akizindua Mtambo huo wenye thamani ya
Dola milioni moja za Kimarekani, Mwenyekiti
wa Baraza la Chuo Kikuu hicho, Dr JUMA
MWAPACHU amesema kuwa licha ya
Kufundishia Chuoni hapo, Mtambo huo
utawanufaisha Watanzania na Wachimbaji wa
kada zote katika kupima na kuonyesha
mahali Miamba ya Madini wanayokusudia
kuichima ilipo.
Akizungumzia manufaa ya Mtambo huo, Dr
MWAPACHU ametaja baadhi ya faida
watakazopata Wachimbaji mbali na Wanafunzi
ambao watajifunza kwa vitendo namna ya
kutafiti Miamba aina mbalimbali kwa ajili ya
Madini, Mafuta na Gesi.
Ili kuhakikisha kuwa Chuo kinajiongezea
mapato kutokana na Mtambo huo, Makamu
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma Profesa
IDRISS KIKULA amesema kuwa Urasimu
kwenye utendaji hautapata nafasi